Amos 6:3-6


3 aMnaiweka mbali siku iliyo mbaya
na kuleta karibu utawala wa kuogofya.

4 bNinyi mnalala juu ya vitanda vilivyofunikwa kwa pembe za ndovu,
na kujinyoosha juu ya viti vya fahari.
Mnajilisha kwa wana-kondoo wazuri
na ndama walionenepeshwa.

5 cNinyi mnapiga vinubi kama Daudi,
huku mkitunga nyimbo za vinanda mbalimbali.

6 dMnakunywa mvinyo kwa bakuli zilizojazwa,
na mnajipaka mafuta mazuri,
lakini hamhuzuniki kwa maangamizi ya Yusufu.
Copyright information for SwhKC